Matamshi ya chuki yaweza kuwa maneno au vitendo vinavyoonyesha hisia za uadui, dhihaka, au kutokuwajali kuelekea mtu au kundi fulani. Yanaweza kujitokeza kwa misingi ya tofauti za kijamii, kitamaduni, kidini, kisiasa, au mambo mengine. Chuki inafarakanisha makundi, huchangia vurugu na migogoro, na hudhoofisha jitihada zetu zote za amani, utulivu na maendeleo endelevu.
Hata hivyo, sasa ukubwa na athari yake umesambazwa zaidi na teknolojia mpya za mawasiliano ambayo sasa yanawafikia watu wengi sana kwa haraka sana.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres anasema "Tunahitaji kuchukulia hotuba za chuki kama tunavyochukulia vitendo vyovyote vibaya: kwa kuzilaani, kutoziendeleza, kukabiliana nazo na ukweli na kuchagiza...