JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums
Huyu ni mnyama mkali sana, mkorofi, na mwenye nguvu katika jamii ya paka. Akiingia bandani, anondoka na kuku mzima na anaenda kula kichwa mpaka shingoni. Kama ni kifaranga, anakula chote au akikuta mayai ambayo bado kidogo ya yaanguliwe, ndio soshi wake. Anakaa vichakani au porini, sehemu yenye msitu mkali. Akigundua kwamba yupo kwenye eneo lenye adui kama mbwa, chui, fisi au binadamu, anaachia ushuzi wake ambao unanukia kama wali au ubwabwa, kiasi kwamba utadhani mtu kaficha huo wali vichakani. Kumekuwa na dhana kwamba ukisikia harufu ya ubwabwa vichakani, ni chatu. Hapana, sio kweli; ni huyu mnyama anayeitwa kanu katika Kiswahili (kwa huku mtaani, sijui upande mwingine). Naendelea kutega; nikikamata nitawaletea mumjue. Huyu...
Chadema imewapiga marufuku maelfu ya watanzania ambao wana elimu ya msingi na kidato cha nne wasigombee uongozi wowote katila chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Chama hicho, japo kimewanyima haki ya kugombea, kinatarajia kwenda kuwaomba kura ili kuwatumia kisiasa kwa faida yao Ni nadra sana kukutana na mjumbe wa serikali ya mtaa au kitongoji mwenye elimu ya kidato cha sita, achilia mbali mwenyekiti wa mtaa na wa kijiji. Sasa ni zamu ya watanzania hao kuwaadhibu chadema kwa dhambi hii ya ubaguzi
Tangu nikiwa mdogo nilisikia na kuamini kwamba ute/ mapovu yanayokuwa kwenye mimea ni mate ya nyoka. Mpaka kufika wakati huu bado sijajua kama suala hili lina ukweli ama la. Naomba wataalamu mnisaidie kujua uhalisia wa jambo hili Kielelezo 1: Picha ikionesha mmea umeachiwa mapovu Kielelezo 2: Picha ikionesha mdudu aina ya Spittlebugs anayetengeneza Povu kwenye mimea Video ikionesha namna wadudu aina ya Spittlebugs wanavyotengeneza povu
Nimeona mtandaoni Mkuu wa kitengo cha Digital, Crown Fm ameandika kuwa Mara ya mwisho Yanga SC kufungwa kwenye Ligi Kuu ni Oktoba 4, 2023 bado siku 3 itimize mwaka mmoja pasipo kupoteza mchezo kwenye Ligi Ligi Kuu ya NBC PL. Eti wadau huyu anasema kweli au anatupanga maana huwa naona kama mnazi wa Yanga isijekuwa mapenzi ya timu yamefanya achakachue takwimu atupange. JamiiCheck fanyenyi jambo tujue Ukweli.
Salama wakubwa wa JamiiCheck? Katika pitapita zangu mitandaoni kuna mtu nimeona akishauri kuwa ni vizuri kumnyoa mtoto mchanga nywele alizozaliwa nazo ili mtoto akue vizuri. Amedai kuwa mtoto asiponyolewa nywele hizo anaweza pata madhara ya ngozi ya kichwa, ukuaji duni lakini mwisho ni mambo ya kiimani. Binafsi nipo njiapanda maana nimekuwa nikiona watoto wengine wakinyolewa ndani ya wiki moja baada ya kuzaliwa, lakini wengine hawajawahi guswa nywele zao mpaka wanakuwa wakubwa.
Wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kikitangaza kufanya Maandamano ya amani leo Jijini Dar Es salaam chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amechapisha mtandaoni mwake akisema anazo taarifa kuwa Mwenyekiti Mbowe yupo Arusha na hivyo kumualika ofisini kwake Jijini Arusha. Makonda ameandika "Kaka yangu Mbowe kumbe umeingia Arusha na hausemi. Karibu Ofisini basi ukiamua Kutoka" Ikumbukwe kuwa saa chache zilizopita, nyumba ya Freeman Mbowe iliyopo Mikocheni ilizingirwa na Jeshi La Polisi huku mkewe Dr Lilian Mtei akiripotiwa kuzuia kutoka nyumbani kwake. Source: Jambo TV
Back
Top Bottom